KLH NewsKLH News Podcast

Where Tanzania is the news!

login to access this featurelogin to access this featuresubscribe using RSS

Episodes:26
Language:en-us
Updated:7 months ago (login to update)
Categories:News

 

Alichozungumza Mhe Zitto Detroit!

audio mp3 - click to play
Published: 7 months ago
Size: 40.9MB


Karibu wiki moja iliyopita Mhe. Zitto Kabwe alizungumza na jumuiya ya Watanzania waishio Jimbo la Michigan nchini Marekani. Mazungumzo hayo yaliyofanyika wakati wa hafla ya chakula cha jioni aliyoandaliwa Bw. Zitto yaligusia mambo mbalimbali na hasa kuwataarifu wanajumuiya hiyo mambo mbalimbali yanayoendelea nyumbani na pia kusikiliza maoni na maswali yao.

Matangazo ya leo basi ni hotuba ya Mhe. Zitto kwa jumuiya hiyo na sehemu ya maswali na majibu, yote ni uncut and an edited. Makosa mengine yoyote ya kurekodi hasa mwanzoni kidogo ni ya KLHN.

Pichani Mhe. ZItto akijiandaa kuzungumza na wanajumuiya ya TAMI - Tanzanians Association of Michigan. Huko Detroit eneo la Maili Nane.


 
 

Nimevunja Mwiko - Soma "Kulikoni" la Leo

audio mp3 - click to play
Published: 7 months ago
Size: 13.0MB


Kwa karibu wiki mbili sasa nimekuwa nikitengeneza hoja na kumulika kama vile kurunzi idara ya Usalama wa Taifa. Sikiliza introduction ya makala yangu maalum kwenye gazeti la "Kulikoni" leo. Kwa wale ambao hampo nyumbani makala hii itawekwa baadaye mchana wa Ijumaa (saa za Marekani) kwenye http://www.klhnews.com upande wa editorial.
 
 

Chenge - mbona anatuchengua!?

audio mp3 - click to play
Published: 8 months ago
Size: 12.0MB


Chenge ni bilionea wa kutupwa ambaye kwake shilingi Bilioni moja anayodaiwa kuificha huko Marekani ni sawa na "vijisenti" vichache. Hivi tatizo letu liko wapi? Je yawezekena kuwa chenge ni dalili tu ya tatizo? Je eye ni kiongozi pekee wa TAnzania ambaye amewekeza mabilioni ya shilingi kwenye akaunti za kigeni? Je ajiuzulu au na yeye anaweza akalia kuwa amefanywa "Bangusilo" wa rada!?
 
 

KLH Exclusive: "Mafuriko Kyela - 40,000 hatarini!" - Dr. Harrison Mwakyembe

audio mp3 - click to play
Published: 8 months ago
Size: 18.3MB


Pichani baadhi ya wananchi wakijaribu kuvuka mto. Kidaraja hicho sasa hakipitiki tena. Picha kwa hisani ya Mjengwa

Mvua za masika zimezidi kupamba moto nchini na zimekuwa zikisababisha mafuriko sehemu mbalimbali. Baadhi ya maeneo ambayo yamepata mafuriko ni pamoja na Vunjo, Same na Kyela. Hata hivyo hadi hivi sasa ni wilaya ya Kyela ambayo ina kata 15 ambazo kati ya hizo 11 zimepatwa na mafuriko makubwa .

Siku ya Jumamosi nimepata nafasi ya kuzungumza na Mbunge wa Jimbo la Kyela Dr. Harrison Mwakyembe (CCM) kuhusu athari za mafuriko hayo na mahitaji ya msaada. Kwa kifupi hali ilivyo ni kuwa:

a. Kaya 9000 hazina mahali pa kuishi, zimekosa chakula, au athari ya moja kwa moja iliyotokana na mafukio hayo

b. Hadi hivi sasa watu wawili wamefariki

c. Madhara makubwa katika mashamba ya mpunga kiasi kwamba kuna uwezekano kuwa kwa mara ya kwanza Kyela itahemea chakula mwaka huu.

d. Mvua kubwa namna hii hazijawahi kunyesha Kyela kwa karibu miaka thelathini sasa.

e. Juhudi za kuleta misaada zinaendelea ambapo JWTZ imepeleka kikosi chake cha Uhandisi, huku Msalaba Mwekundu wakiandaa misaada ya vitu mbalimbali.

Dr. Mwakyembe anaomba msaada wa Watanzania wote popote pale walipo kuweza kusaidia wananchi wenzao ambao ni kama wamepatwa na "Kimbunga cha Katrina" kwani wengi sasa wanaishi makanisani na kwenye mashule na afya zao ziko hatarini hasa kutokana na uwezekano mkubwa wa kuibuka mlipuko wa magonjwa yanayoambukizwa kwa maji kama typhoid, kuhara damu, salmonella, na pia ongezeko la Mbu wasababishao Malaria.

Kwa yeyote aliyeko Dar, unaweza kutuma mchango wako kupitia:

Kyela Development Fund MNB Bank House Acct No: 2013300198

Au Wasiliana na Dr. Mwakyembe kupitia simu Namba: 255 754 284130

kwa maelekeo ya kuweza kutoa mchango wako kupitia yeye mwenyewe

Tafadhali sikiliza mahojiano yangu na Dr. Mwakyembe. KLH News imeahidi kutoa msaada wa Shilingi laki mbili kama sehemu ya jitihada za kuwasaidia wananchi wa Kyela


 
 

Bila CCM Madhubuti? - Mwalimu alisema kweli...

audio mp3 - click to play
Published: 8 months ago
Size: 20.1MB


Mwanzoni sikuyaelewa maneno ya Baba wa Taifa Mwl. J.K. Nyerere kuwa “Bila CCM Madhubuti nchi yetu itayumba”. Nilifirikia kuwa alimaanisha “Bila CCM” nchi yetu itayumba, na pia nilidhania alimaanisha kuwa “Bila viongozi wa CCM” nchi yetu itayumba. Miaka hii ilivyopita na hasa baada ya matukio yaliyolikumba Taifa letu ndio maana hasa ya maneno yake imeanza kuniingia na kwa hakika nimekubali kuwa bila Chama cha Mapinduzi ambacho ni “madhubuti” basi Taifa letu liko matatani, na kwa hakika litayumba.

Kabla hujaanza kunirarua nisikilize hapa au kwenye http://www.klhnews.com


 
5 of 26 episodes displayed
View All Episodes >
(21 more)

Comments

- no comments found -


Login to post a comment

What's Hot

phpBB Podcast -Cambridge Riffs: Podcast Radio for Cambridge- BendingCorners : jazz-n-groove Animal Wise Radio Podcast AP NewsPulse Baby Boomer Librarian Career Opportunities TPN :: The AFL Show Modern Office Furniture Bertone Beatle Bonanza Tech Talk for Families: mp3 Russell Brand

What's New

Don’t Give Me Excuses! Wood Rot Johnson County, KS Painting Contractor - Johnson County, Kansas Exterior Painter Colon Health Cleanse Modern Office Furniture Business and Personal Coaching Seminar Prince Edward Island Songwriter Series Sylver Tarot How to Meditate; Ways to Meditate Are you trying to make money online? You can bring money to your bank account today!! Day 19 Response to Dennis Karganilla's 90 Day Challenge Essential Advice about Network Marketing & MLM for Your Success! Quick Cheap And Easy Money Making Program!

Recently Updated

AME Info Video Cast 5th Element Podcast Bob & Sheri Podcast Funny Cartoon Podcast: THE BAKERS The Lippis Report Podcast The Restaurant Guys Value Line Observer by the Value Guys! Life Matters EconTalk Nightlife with Tony Delroy. Mary Murphy Tells Stories Gameday Audio Rewind